Top Stories

Davido ashikiliwa na kuhojiwa na polisi….kisa?

on

Polisi katika mji wa Lagos nchini Nigeria wamemshikilia kwa masaa kadhaa mwanamuziki maarufu nchini humo Davido ili kumhoji kuhusiana na kifo cha rafiki yake aliyefariki katika mazingira ya kutatanisha mnamo October 3 mwaka huu.

Imeelezwa na msemaji wa polisi hao kuwa Davido sio mshukiwa wa kifo hicho moja kwa moja lakini ameitwa ikiwa ni pamoja na ndugu wa marehemu huyo ili watoe maelezo ya wanachokifahamu kuhusu utata wa kifo hicho ikiwa ni pamoja na kueleza walikua wapi siku ya tukio.

Marehemu Tagbo Umeike aliuawa na mwili wake kuachwa nje ya hospitali mjini Lagos. Davido amekana kabisa kuhusika na kifo hicho.

Ulipitwa na hii? EXCLUSIVE: Mwanafunzi aliyezawadiwa gari na Shule kaongea

Soma na hizi

Tupia Comments