Michezo

Ulimwengu ang’aa TP Mazembe

on

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars na club ya TP Mazembe ya Congo Thomas Ulimwengu amezidi kung’aa katika Ligi Kuu ya Congo baada ya kuipatia ushindi timu yake ya TP Mazembe wa goli 1-0 dhidi ya Dauphin Noir.

Goli hilo la Ulimwengu linamfanya afikishe jumla ya magoli manne katika Ligi Kuu ya Congo msimu wa 2020/21 akiwa nafasi ya pili kwa vinara wa magoli wa kwanza akiongoza kwa kuwa na magoli 5 katika Ligi Kuu Congo (Ligue 1).

Ulimwengu sasa toka arejee TP Mazembe baada ya kuwa na kiwango cha kupanda na kushuka sababu ya jeraha la goti, sasa amerejea katika uwezo wake na kuwa tumaini kwa TP Mazembe.

Soma na hizi

Tupia Comments