Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es salaam limewahakikishia ulinzi na usalama wakazi wote wa Dar es salaam na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CHADEMA utakaofanyika kesho kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi wao wakuu wa chama hicho utakao fanyika katika ukumbi wa Mlimani City.
Ameyasema hayo Kamanda wa kanda maalum SACP Jumanne Murilo na kusema watu wote watakao kuwepo katika ukumbi wa Mlimani city wanapaswa kuwa salama kama wananchi wengine wa mkoa wa Dar es salaam hivyo watapewa ulinzi kabla ya kikao hicho na baada ya kikao hicho kwasababu hiyo ni kazi yao.