Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprisca Mahundi ameitaka jamii kushirikiana na viongozi wa kisekta, watetezi wa Faragha na uhuru wa Raia ili kuwa na taifa linaloheshim faragha na kuwalinda watumiaji wa Taarifa kwenye uchumi unaendeshwa na Taarifa.
Mhandisi Mahundi ametoa wito huo Novemba 15, 2024 jijini Arusha wakati akifunga kongamano la Anuai za kitaaluma lililoandaliwa na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TSL)kwa kushirikiana na tz_privacy_professionals ambapo amesema Ulinzi wa Taarifa ni wa kila mtu na sio wa Serikali peke yake.
“Suala la Ulinzi wa Taarifa na la kila Mmoja wetu na sio la Serikali Peke yake kwani tunaishi katika enzi ambapo Taarifa hutiririka katika tania, mipaka na mifumo ya ofisi kwa kasi kubwa hivyo tunatarajia kushiriki kwa pamoja sisi kama Serikali pamoja na wadau mbalimbali katika kufika malengo tulijowekea” amesema Mhandisi Mahundi
Katika hatua nyingine Mhandisi Mahundi akatumia Jukwaa hilo kukipongeza Chama cha Wanasheria Tanganyika kwa kuandaa kongamano hili na kuwataka Wanasheria nchini kuisadia Serikali katika kusimamia Sheria na utekelezaji wa sera mbalimbali za Ulinzi wa Taarifa nchini.
“Tunatarajia Wanasheria mtatusaidia katika kusimamia sheria na Sera mbalimbali zinazosimamia Ulinzi wa Taarifa ili kuimarisha hatari tunazokabiliana nazo kama vile ukiukwaji wa Faragha na Mashambulizi ya Kimtandao” amesema MhandisiMahundi
Kongamano hili la siku tano (5) lililobebwa na kauli mbiu ya Ulinzi wa Taarifa katika Uchumi wa Sekta mbalimbali kujenga njia iliyo ya Faragha na Usalama limewakuwakutanisha pamoja wataalamu kutoka sekta mbalimbali nchini na kujadili kwa kina kuhusu dhana ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.