Ni Julai 19, 2023 ambapo Kampuni Binafsi za Ulinzi nchini zimetajwa kuwa na mchango mkubwa katika masuala ya ulinzi shirikishi kwenye jamii hivyo wasimamizi wa Kampuni hizo kutakiwa kusimamia taratibu za utoaji wa mafunzo kwa watendaji wao ili kuongeza ufanisi unaotakiwa katika kazi ya ulinzi ndani ya Jamii.
Wito huo umetolewa Jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Ushirikishwaji Jamii Mkoa wa Kipolisi Temeke ACP Emma Foya wakati wa mkutano maalumu wa Umoja wa Kampuni Binafsi za Ulinzi Kanda ya Pwani uliowakutanisha wakurugenzi wa Kampuni mbalimbali kujadili changamoto zinazoikabili tasnia hiyo ziweze kupatiwa ufumbuzi.