AyoTV

VIDEO: Zaidi ya shilingi Trilioni moja kutengwa kwa ajili ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa

on

Mei 10 2016 Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa imewasilisha hotuba yake ya mapitio ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2016/2017 ambayo imesomwa na Waziri wake Hussein Mwinyi ambaye amesema…

>>‘Wizara yangu inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kupatiwa kiwango pungufu cha fedha ikilinganishwa na mahitaji halisi ambayo ni makubwa

Hali ya kutengewa bajeti ndogo na  fedha pungufu imekuwa ikiathiri utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya Jeshi na pia kusababisha ulimbikizaji wa madeni hususani ya kimkataba ambayo tumeingia na makampuni mbalimbali kwa ajili ya kuliwezesha Jeshi kizana na kivifaa

Mpango wa utekelezaji wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa wa mwaka 2016/2017 umekusudia kuimarisah utekelezaji kazi na ufanisi wa Jeshi kulingana na Dira na Dhima ya Wizara

Ili Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa na Taasisi zake iweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo katika mwaka 2016/2017 naliomba Bunge liidhinishe jumla ya shilingi 1,736,530,000.00 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na matumizi mengine 

ULIIKOSA HII NAIBU WAZIRI POSSI BUNGENI KUHUSU MILIONI 50 ZA RAIS MAGUFULI KILA JIJIJI?

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments