Umoja wa Mataifa umetoa dola milioni 15 za kimarekani kwa mwitikio wa dharura wa kukabiliana na mafuriko makubwa ambayo yamewaathiri watu zaidi ya laki 7 nchini Sudan Kusini.
Mratibu wa Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini Bi Anita Kiki Gbeho, amesema dola milioni 10 za kimarekani kutoka Mfuko wa Mwitikio wa Dharura wa Umoja wa Mataifa CERF zitatumiwa kutoa msaada kwa wale walioathiriwa na mafuriko makubwa katika kaunti tano zilizoathiriwa vibaya zaidi.
Bi Gbeho ametenga dola nyingine milioni 5 za kimarekani kutoka Mfuko wa kibinadamu wa Sudan Kusini, ili kuongeza kwenye dola milioni 10 za kimarekani kutoka mfuko wa CERF, ikilenga kuimarisha mabomba makuu ya kukabiliana na mafuriko na huduma za kwanza.
Bi Gbeho ametoa taarifa ikisema mafuriko yameharibu maisha ya watu kote nchini Sudan Kusini.