Mix

‘Umebaki mwezi mmoja itatua ndege ya Diamond’- Meneja Sallam

on

Meneja wa Msanii Diamond Platnumz,Sallam SK amesema kuwa umebaki mwezi mmoja tu itatua ndege ya Msanii Diamond Platnumz na kinachofanyika sasa ni makubaliano ya mwisho kuweza kuichukua.

Kupitia Interview ambayo ameifanya Sallam SK  July 20, 2021 katika kipindi cha The Switch amesema kuwa wiki inayofuata wamealikwa kwenda kuikagua na pia tayari zimetumwa picha za awali zikionesha muonekano wake wa ndani na nje kutoka kwa wakala atakayeuza ndege hiyo.

Watu wanaweza kusema ndege pia iwe ya mwaka 2021 lakini kwenye hili naomba watusamehe, sisi tutanunua ndege na tunachohakikisha tumetimiza lengo katika hili – amesema meneja Sallam

Tupia Comments