Serikali kupitia TANESCO imekamilisha miradi mitano na inatekeleza miradi mingine saba ya kufua umeme kwa kutumia nishati ya gesi asilia mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara na Lindi.Kiasi cha umeme unaofuliwa kwa kutumia gesi asilia unafikia megawati 546 na miradi iliyopo kwenye utekelezaji itakapokamilika inatarajiwa kuongeza ufuaji wa umeme kutokana na gesi asilia kufikia megawati 2,475.Miradi hii ipo kwenye hatua mbalimbali.
Leo Octoba 13 TANESCO ilizindua rasmi mradi huo wa Umeme unaozalishwa kutokana na gesi asilia ambapo katika uzinduzi huo mgeni rasmi alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.
Kukamilika kwa miradi hiyo kutakidhi mahitaji ya umeme nchini na kuondoa utegemezi wa mitambo ya kufua umeme kwa njia ya maji ambayo kiwango cha ufuaji wa umeme kimeshuka kutokana na kushuka kwa kina cha maji kwenye mabwawa, hali ambayo kwa kiwango kikubwa imesababishwa na mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na kuendelea kwa shughuli za kibinadamu kwenye mito inayotiririsha maji kwenye mabwawa hayo.
“Niliagiza lazima Makao Makuu ya Wilaya zote kuunganishwe Umeme, zimebaki Wilaya mpya chache ambazo bado”- #RaisJK #UmemeKINYEREZI
— millard ayo (@millardayo) October 13, 2015
“Upatikanaji wa Umeme tuliupa kipaumbele kwa kuwa tunajua hakuna Maendeleo bila Umeme”- #RaisJK #MillardAyoUPDATES #UmemeKINYEREZI — millard ayo (@millardayo) October 13, 2015
“Tuna mpango wa kuifanya Tanzania ya Viwanda ndio maana tunaimarisha Miundombinu ikiwemo Umeme wa uhakika”- #RaisJK #UmemeKINYEREZI
— millard ayo (@millardayo) October 13, 2015
“Kuna upungufu mkubwa wa umeme kwa sababu mabwawa yanazalisha chini ya kiwango”- #RaisJK #MillardAyoUPDATES #UmemeKINYEREZI — millard ayo (@millardayo) October 13, 2015
Kiwango cha umeme kinachozalisha kutokana na vyanzo vya maji ni Megawati 561.Miradi inayotekelezwa katika kituo cha kinyerezi pekee ni minne (4), Kinyerezi 1, Kinyerezi 2, Kinyerezi 3, Kinyerezi 4.Miradi mingine miwili inatekelezwa mkoani Lindi ambayo ni Kilwa Energy na Kilwa Power Plan.Mradi mmoja utatekelezwa mkoani Mtwara.
Rais JK: “Nawapongeza TANESCo kwa Ujenzi wa Kituo cha ‘Kinyerezi I’, tulikuwa na tatizo la umeme lakini Gesi itasaidia kumaliza tatizo”
— millard ayo (@millardayo) October 13, 2015
Rais JK: “Nawapongeza TANESCo kwa Ujenzi wa Kituo cha ‘Kinyerezi I’, tulikuwa na tatizo la umeme lakini Gesi itasaidia kumaliza tatizo” — millard ayo (@millardayo) October 13, 2015
“Lengo ni kufikisha Uzalishaji wa Megawati 2,700 mpaka mwaka 2016,kwa sasa tunazalisha Mg 1,390”- #RaisJK #MillardAyoUPDATES #UmemeKINYEREZI
— millard ayo (@millardayo) October 13, 2015
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram naYouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.