Mix

‘Hadi sasa Tanzania tunanunua umeme toka Uganda, Zambia na Kenya’ – Prof. Muhongo

on

Ni waziri wa nishati na madini Profesa Sospeter Muhongo akiongelea yaliyozungumzwa kwenye kikao cha ushirikiano wa nchi za Afrika Mashariki ambao lengo lake ni kusaidia nchi hizi kupata umeme mwingi wa uhakika na wa bei nafuu.

Sasa ili tuyapate hayo matatu tunalazimika kuwa kama nchi nyingine duniani ambazo zinauziana umeme, ndugu zangu Watanzania hadi sasa hata sisi Tanzania tunanunua umeme kutoka Uganda karibu megawati 17, kutoka Zambia Megawati 4 na Kenya tunanunua megawati 1‘ – Profesa Muhongo

Huko tunakokwenda Afrika Mashariki ijayo na Afrika kwa ujumla tumeamua kujenga miundombinu ya kusafirisha umeme mwingi kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine, sasa hivi kama mnafatilia tumeanza kujenga njia ya kusafirisha umeme kutoka Singida kwenda Kenya ya Kilovoti 400‘ – Prof. Muhongo

Makusudio ya kujenga njia hizi ya kusafirisha umeme mwingi ni kwamba muda umefika nchi za kiafrika tuuziane umeme, badala ya kununua umeme wa bei mbaya wa mafuta hapa Tanzania… huo umeme tunaweza tukaununua Uganda au Ethiopia, kikao chetu hiki kilikua kinajadili miradi ambayo tulikua tunapaswa kuitekeleza‘ – Profesa Muhongo

Soma na hizi

Tupia Comments