WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu amesema kuwa matumizi ya Nishati ya kuni na mkaa yamekuwa yakisababisha madhara ya saratani ya mfumo wa chakula hivyo wakati umefika wa kutumia nishati ya gesi ili kujiepusha na madhara ya kiafya.
Waziri Ummy ameyasema hayo wakati wa ugawaji wa majiko ya gesi Kwa wajasiriamali 600 wa Jiji la Tanga ikiwa ni mkakati wa kuendelea kuhamasisha jamii kutunza mazingira.
Alisema kuwa matumizi ya nishati mbadala ndio ambayo yatatoa uhakika wa afya za Wananchi lakini yataweza kutulinda dhidi ya majanga ya mabadiliko ya tabia Nchi ambayo yameikumba dunia kwa Sasa.
“Mitungi hii tuliyopewa na kampuni ya Oryx Gas tunaigawa Kwa Wanawake wajasiriamali Kwa lengo la kupunguza gharama za mkaa na Kuni lakini na kuhamasisha matumizi ya gas kama nishati mbadala kwenye mapishi”– alisema Waziri Ummy.
Alisema kuwa mitungi hiyo yenye thamani ya sh Mil 51 ambayo imegaiwa Bure Kwa wajasiriamali hao Ili kuwarahisishia shughuli zao za biashara.
Nae Mkurungenzi Mkuu wa Oryx Gas .Araman Benoite amesema kuwa msaada huo ni unalenga kuhamasisha matumizi ya gesi Ili kulinda mazingira yetu ikiwemo kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi.