Top Stories

Ummy awa mkali “hatutaki mambo ya uhuni, RC wakapeleke ndani” (+video)

on

Waziri wa Nchi TAMISEMI Ummy amewakabidhi Mikononi mwa Polisi viongozi wa Kijiji cha Nyamililo Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema Mkoni Mwanza kwa kuchangisha wananchi michango bila Kibali cha Mkuu wa Wilaya.

Waziri Ummy amechukua hatua hiyo wakati wa ziara yake Wilayani humo ambapo alitembelea Zahanati ya Nyamililo kukagua maendeleo ya ujenzi.

Akiwa Zahanati ya Nyamalilo alibaini kuwa TAMISEMI imeleta fedha za kukamilisha Zahanati hiyo Shilingi Mil 50 ambazo kwa hali ya Zahanati ilivyokua ingekamilika na Fedha kubaki lakini Viongozi hao wa Kijiji waliendelea kuwachangisha wananchi sh 9,500 kwa Kaya kwa madai wanakamilisha Zahanati hiyo.

 

Soma na hizi

Tupia Comments