Ripoti ya karibuni zaidi ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya hewa ya sayari ya dunia ilichapishwa siku Jumatatu, na mbali na kuonya tena kuhusu ongezeko linaloendelea la joto duniani, imewanukuu wanasayansi wakitahadharisha kwamba binadamu watakuwa katika hatari kubwa iwapo ongezeko la joto litapita kiwango cha sasa.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres ameonya katika mkutano wa wiki moja kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa huko Interlock, Uswisi, kwamba sayari ya dunia inakaribia hatua ya kuangamia na kwamba nchi za dunia zinapaswa kutekeleza makubaliano ya kupunguza nyuzi joto moja na nusu.
Itakumbukwa kuwa, Mataifa ya dunia yalikubaliana miaka minane iliyopita mjini Paris kujaribu kuplibalisha joto hadi kwenye nyuzi joto 1.5, au angalau kuliweka chini ya nyuzi joto 2.
Wastani wa joto duniani umeongezeka kwa nyuzi joto 1.1 tangu karne ya 19, lakini Guterres amesisitiza wiki iliyopita kwamba lengo la 1.5C linawezekana kwa kupunguzwa kwa kasi na kwa kina uzalishaji wa hewa chafu katika sekta zote za uchumi wa dunia.