Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa imesema kuwa, takriban watu milioni 258 wa 58 duniani walikumbwa na uhaba mkubwa wa chakula mwaka jana kutokana na migogoro, mabadiliko ya hali ya hewa, athari za janga la janga la corona na vita nchini Ukraine. Kwa mujibu wa ripoti hiyio, hilo ni ongezeko kubwa ikilinganishwa na watu milioni 193 walioukumbwa na njaa mwaka wa kabla yake.
Taarifa ya taasisi ya Ripoti ya Kimataifa ya Migogoro ya Chakula ya Umoja wa Mataifa ndiyo iliyotangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, watu walioathiriwa zaidi na njaa na vifo ni wa nchi saba ambazo ni Somalia, Afghanistan, Burkina Faso, Haiti, Nigeria, Sudan Kusini na Yemen.
Ripoti hiyo imefichua kuwa idadi ya watu wanaokabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula na wanaohitaji msaada wa haraka imekuwa ikiongezeka kwa mwaka wa nne mfululizo.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema: “Kuongezeka umaskini, kukosekana usawa, kukithiri maendeleo duni, mzozo wa hali ya hewa na majanga ya asili pia huchangia uhaba wa chakula duniani.”
Rein Paulsen, mkurugenzi wa masuala ya dharura wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, amesema, matatizo mengi yanayoingiliana ni sababu la kuongezeka baa la njaa.
Migogoro mbalimbali, majanga ya hali ya hewa, athari za ugonjwa wa corona na matokeo mabaya ya vita vya Russia na Ukraine ambavyo vimeathiri biashara ya kimataifa ya mbolea, ngano, mahindi na mafuta ya alizeti ni miongoni mwa sababu la ongezeko hilo kubwa la watu waliokumbwa na baa la njama mwaka 2022. Athari zake ni kubwa zaidi katika nchi maskini ambazo zinategemea uagizaji wa chakula kutoka nje.
Paulsen amesema: “Bei za mahitaji muhimu zimeongezeka na kuziathiri vibaya nchi hizo maskini.”
Vile vile ametoa mwito wa ufadhili zaidi katika sekta ya kilimo ili kupambana na mgogoro wa chakula.