Top Stories

Rais Magufuli amefanya tena uteuzi mwingine leo August 11, 2017

on

Rais Magufuli leo August 11, 2017 amemteua Dkt. Hassan Abbas kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari, Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Dkt. Hassan Abbas umeanza tarehe 09 Agosti, 2017.

Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Hassan Abbas alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Maelezo na aliteuliwa kushika nafasi hiyo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma namba 8 ya mwaka 2002.

Dkt. Hassan Abbas ameteuliwa kushika nafasi hiyo kwa mujibu wa Sheria Mpya ya Huduma za Vyombo vya Habari ya mwaka 2016, ambapo nafasi hiyo imebadilishwa kutoka Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Maelezo na kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari, Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali na Mamlaka ya uteuzi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

“Ameamua mwenyewe kutuletea hizi fedha…” – Rais Magufuli…

Soma na hizi

Tupia Comments