AyoTV

Maamuzi ya Mahakama ya Kisutu kuhusu Mkutano wa Simba SC August 13

on

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu usiku wa jana iliyatupilia mbali maombi ya Bodi ya Wadhamini wa Klabu ya Simba walioomba kusitisha Mkutano Mkuu wa Jumapili Agosti 13, 2017.

Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amesema anakubaliana mapingamizi ya wajibu maombi kwamba wapo baadhi ya wajumbe wameanza kufika Dar es Salaam na kwamba Klabu hiyo imelipia ukumbi akiongeza kuwa ameona gharama isiwe kubwa na kwamba waleta maombi wanaweza kupeleka malalamiko yao katika mkutano huo.

GOAL: Ushindi wa Simba vs Rayon Sports, Simba Day 8 2017 Full Time 1-0!!!!

Soma na hizi

Tupia Comments