Leo August 8, 2017 Kenya imefanya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Magavana wa Kaunti, Wabunge, Maseneta, Wawakilishi wa Wanawake, Wawakilishi wa Wadi.
Moja ya matukio yaliyoambatana na zoezi hilo ni mwananmke mmoja anayeitwa Paulina Chemanang ambaye alikuwa na ujauzito aliiambia Radio ya Capital FM kuwa hakujisikia maumivu wakati alipofika kujipanga kupiga kura katika kituo cha kupigia kura cha Kaunti ya Pokot Magharibi.
>>>”Sikuhisi maumivu, niliyahisi muda mfupi baada ya kuwasili hapa. Sikuhisi chochote tangu jana.”
Paulina alisema alihisi maumivu ya uchungu muda mfupi baada ya kuwasili kituoni na kwa msaada wa watu waliokuwa karibu, alijifungua mtoto wa kike kisha alipelekwa Kituo cha afya cha karibu na baadaye alirejea kupiga kura.
Mwanamke mmoja amejifungua mtoto leo akiwa kwenye mstari akisubiri kupiga kura Kenya, alihakikisha amepiga kura yake. #MillardAyoUPDATES. pic.twitter.com/lm5IKTyoXN
— millardayo (@millardayo) August 8, 2017