Michezo

Watanzania wawili wametangazwa mamilionea, serikali kuvuna Tsh milioni 160

on

Baada ya kuanzishwa 2017 kampuni ya michezo ya ubashiri ya SportPesa nchini Tanzania, hatimae leo imefanikiwa kupata washindi wawili waliofanikiwa kubashiri game 13 kwa ufasaha katika Jackpot.

Hii ndio kwa mara ya kwanza nchini Tanzania katika michezo ya ubashiri mtu au watu kushinda zaidi ya Tsh milioni 825 kwa kubashiri tu.

Washindi wa SportPesa ni wawili akiwemo Simon Pascal kutokea Biharamuro mwenye umri wa miaka 26, ushindi huo utapelekea serikali ya Tanzania kupata zaidi ya Tsh milioni 160 kama kodi, washindi hao wametangazwa na mkurugenzi wa utawala na utekelezaji Abbas Tarimba.

Soma na hizi

Tupia Comments