Michezo

Unaambiwa hili ni moja ya magoli bora kabisa ya Ronaldo – litazame hapa

on

Screen Shot 2014-05-05 at 5.20.30 AMCristiano Ronaldo jana aliwezesha timu ya Real Madrid kuendelea kuwa kwenye mbio za ubingwa baada ya kuifungia bao muhimu la kusawazisha dhidi ya Valencia kwenye ligi kuu ya Hispania – La Liga.

Mpaka kufikia dakika ya 90, Real Madrid walikuwa nyuma kwa mabao 2-1 baada ya Parejjo na Mathieu kuwafungia Valencia mabao mawili, Sergio Ramos akasawazisha lakini mambo yakaendelea kuwa magumu kwa Madrid.

Wakati baadhi ya mashabiki wakiwa wanaondoka uwanjani Cristiano Ronaldo alipokea krosi kutoka kwa Di Maria na akafunga goli kwa kisigino akiwa amelipa mgongo goli la Valencia.

Tupia Comments