Mix

Unajua Januzaj amesema nini kuhusu malengo yake na Juan Mata?

on

352899_heroa

Ikiwa leo ni siku ambayo anatimiza miaka 19 tangu kuzaliwa kwake, kinda la Manchester United  Adnan Januzaj ameongelea malengo yake katika klabu hiyo.

Adnan ambaye alianza rasmi kuichezea timu ya kwanza ya Man United mwanzoni mwa msimu huu amekuwa mmoja wa wachezaji muhimu wa klabu hiyo akiwa tayari ameshacheza mechi 17 katika premier league.

Mchezaji huyo ambaye anagombewa na takribani timu nne za taifa aweze kuzitumikia, jana alipigiwa kura na mashabiki wa Man U ulimwenguni kote kuwa mchezaji bora wa mwezi January.

Akizungumzia malengo yake katika klabu hiyo, Januzaj alisema, “Nimefurahishwa sana na mambo yalivyoenda mwaka huu, nimefanya kazi kubwa kuingia katika kikosi cha kwanza. Nimecheza mechi nyingi na naamini nikiendelea kujituma kuna mengi mazuri yanakuja. Matumaini yangu ni kushinda vikombe nikiwa na timu hii pia kuwa mchezaji bora kabida,” Aliiambia website rasmi ya Manchester United.

Alipoulizwa maoni yake kuhusu usajili wa kiungo Juan Mata, Januzaj alikiri kwamba anategemea kujifunza mengi kutoka kiungo huyo wa kihispania.

“Ni mchezaji mzuri sana na nafikiri nitajifunza mengi sana kutoka kwake.

“Ni fundi wa soka mwenye akili sana uwanjani. Anafunga magoli na kutoa pasi za magoli. Tuna furaha kuwa na Mata kwenye klabu hii.”

Tupia Comments