Dimitar Berbatov amezungumza kwa mara ya kwanza kuhusu uhamisho wake wa kutoka Fulham kujiunga na Monaco akisema kwamba mchezaji mwenzie wa zamani wa Manchester United Patrice Evra alisaidia katika kumshawishi ajiunge na klabu hiyo ya matajiri wa Monaco katika siku ya mwisho ya usajili.
Evra ambaye alitengeneza jina lake akiwa na klabu hiyo ya Monaco, na ndio aliyemshawishi Berbatov, 33, kwenda mkopo kwa Monaco inayotumia dimba la Stade Louis II.
“Niliongea na Evra, aliniambia vitu vingi vizuri kuhusu hii timu,” alisema Berbatov. “Sio kila mtu anakuja uwanjani, lakini timu ipo nafasi ya pili na kwa sasa lengo ni kufuzu kucheza ligi ya mabingwa wa ulaya. Nawafahamu Ricardo Carvalho, ambaye nilicheza dhidi yake nchini England, na sijisikii kama ni mgeni hapa.”