Top Stories

“Unamuita baby, honey halafu unamuua kwa shoka, wivu wa kipumbavu” RPC (+video)

on

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Jonathan Shanna amesema Jeshi hilo litatumia njia mbalimbali ikiwenmo Mabomu ya machozi kumsaka kijana  Latiaeli Pallangyo (28) ambaye anatuhumiwa kwa kumuua mpenzi wake Marry Richard kwa kumkata na shoka siku ya Disemba 25, 2019.

Akizunguza na waandishi wa habari jijini Arusha RPC Shanna amesema “chanzo cha tukio hili ni ugomvi wa kifamilia baina ya wawili hao. Mtuhumiwa alitoroka mara baada ya kufanya tukio hilo na tayari tumeanza kufanya msako mkali wa kumtafuta kwa kushirikna na vyombo vingine vya dola. Tunawaomba wananchi kuwa watulivu na wale wenye taarifa kuhusiana na tukio hili wasisite kutoa ushirikiano.”

MTOTO WA MWAKA 1 AFUKIWA KICHWA CHINI KIWILIWILI JUU

Soma na hizi

Tupia Comments