Top Stories

Undertaker astaafu mieleka

on

Kuna hii ya kuifamu leo November 23, 2020 inayomhusu mchezaji maarufu wa mchezo wa mieleka- Undertaker ambaye amethibitisha rasmi kujiuzulu kutoka WWE baada ya miaka 30.

Aliingia ulingoni kwa mchezo wa mwisho katika mchezo wa mwisho wa Survivor Series Jumapili usiku, ambapo aliuhutubia umma wa mashabiki wa WWE Universe kwa mara ya mwisho.

Wakati wa hotuba yake, Undertaker ambaye jina lake halisi ni Mark Calaway –alieleza ni kwanini ameamua kujiuzulu.

“Kwa miaka 30 nimekuwa nikiingia ndani ya ulingo huu taratibu na kuwaangusha watu mara kwa mara,” alisema, sasa wangu muda umefika. Muda wangu umefika wa kumuacha Undertaker apumzike… kwa … amani,”.

Calaway anajiuzulu akiwa ndiye mchezaji bora wa WWE kuwahi kushuhudiwa katika mashindano hayo na amekuwa ulingoni kwa miongo mitatu na atakumbukwa na mashabiki wake daima.

TANZANIA YAANZA VIZURI MASHINDANO YA CECAFA,YAWACHAPA DJIBOUTI MABAO 6-0

Soma na hizi

Tupia Comments