Kamati ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa (UNECA) imezindua mradi wa kuunga mkono nchi za Afrika kukusanya data za usimamizi kuwa za kisasa kwa ajili ya mchakato wa uzalishaji.
Taarifa iliyotolewa na Kamati hiyo imesema, mradi huo ni mwendelezo wa Njia ya Mageuzi na Usasa wa Takwimu Rasmi barani Afrika kwa mwaka 2023 hadi 2030, ambao ulipitishwa katika Mkutano wa Mawaziri wa Fedha na Uchumi wa UNECA uliofanyika wiki iliyopita.
Akizungumza katika warsha ya siku tatu inayofanyika mjini Yaounde, Cameroon, Mkuu wa Ofisi ya UNECA kanda ya Afrika ya Kati Adama Coulibaly amesisitiza haja ya mfumo wa takwimu wa kitaifa kubadilishwa na kuwa wa kisasa ili kuwa nyumbufu zaidi na kuhimili migogoro.