Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) jana Jumatano liliomba ufadhili wa dola milioni 21.4 za kimarekani kuwasaidia watu milioni 9.9 waliolazimika kukimbia makwao katika nchi 35 za Afrika.
UNHCR limesema fedha hizo zinalenga kuongeza mwitikio muhimu kwa wakimbizi katika nchi zilizoathiriwa na dharura ya homa ya Mpox, na pia zitatumika kuhakikisha wakimbizi na watu waliolazimika kukimbia makwao wanajumuishwa katika mipango ya misaada inayoongozwa na serikali.
Kwa mujibu wa shirika hilo, watu 88 wamegunduliwa kuambukizwa homa ya Mpox miongoni mwa wakimbizi barani Afrika, na 68 kati ya yao wamegunduliwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.