Kumekuwa na Headlines za story nyingi kutoka Kenya zinazohusu mashambulizi ya kigaidi katika maeneo mbalimbali ambapo matukio hayo yanahusisha sana kikundi cha Kigaidi ccha Al-Shabaab, leo kuna tukio jingine kwenye Headlines kuhusu mashambulizi ya aina hiyo.
Ripoti iliyotoka mpaka sasa inasema watu wawili wameuawa na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa kutokana na tukio la uvamizi Garissa College University, walioshuhudia wanasema watu waliovamia haijafahamika idadi kamili ila ni kati ya watu sita na kumi.
Wavamizi hao walikuwa na silaha ambapo imesikika milio ya risasi kutoka kwenye Chuo hicho kilichopo karibia na mpaka wa Kenya na Somalia.
#GarissaAttack According to CEC Health 30 casualties taken to hospital. 4 are very serious. Majority of Casualties have gunshot wounds.
— Kenya Red Cross (@KenyaRedCross) April 2, 2015
#Alert: Armed attack at Garissa University College. @EMS_Kenya and #RedCross Garissa team at scene. Updates to follow
— Kenya Red Cross (@KenyaRedCross) April 2, 2015
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook