Mix

Uvamizi wa kigaidi kwenye Headlines Kenya.. Hii imetokea Chuo Kikuu leo

on

IMG_20150402_090358Kumekuwa na Headlines za story nyingi kutoka Kenya zinazohusu mashambulizi ya kigaidi katika maeneo mbalimbali ambapo matukio hayo yanahusisha sana kikundi cha Kigaidi ccha Al-Shabaab, leo kuna tukio jingine kwenye Headlines kuhusu mashambulizi ya aina hiyo.

Ripoti iliyotoka mpaka sasa inasema watu wawili wameuawa na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa kutokana na tukio la uvamizi Garissa College University, walioshuhudia wanasema watu waliovamia haijafahamika idadi kamili ila ni kati ya watu sita na kumi.

Wavamizi hao walikuwa na silaha ambapo imesikika milio ya risasi kutoka kwenye Chuo hicho kilichopo karibia na mpaka wa Kenya na Somalia.

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Soma na hizi

Tupia Comments