Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) Catherine Russell ameonya kuwa, mapambano ya kijeshi yanayoendelea nchini Sudan yanawaweka hatarini mamilioni ya watoto.
Katika taarifa yake, Russell amesema, mapambano ya siku tano nchini Sudan yameathiri vibaya idadi kubwa ya watoto nchini humo, na kama ghasia hazitasimamishwa, idadi hiyo itaendelea kuongezeka.
Takriban watoto tisa wameripotiwa kuuawa na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa katika mapigano hayo yanayoendelea katika miji ya Khartoum, sehemu ya Darfur na Kordofan Kaskazini.
Russell pia amesema, wamepokea ripoti kuhusu watoto kujihami shuleni na vituo vya kutolea huduma, huku hospitali za watoto zikilazimika kuhamishwa na vituo vya afya na miundombinu mingine muhimu kuharibiwa au kuteketezwa, hivyo kupunguza upatikanaji wa huduma muhimu za kuokoa maisha na dawa.
Ameongeza kuwa mapambano hayo yamevuruga huduma muhimu za kuokoa maisha kwa watoto takriban 50,000 wenye