Duniani

Utata kwenye stage ya fainali za Miss Universe Marekani baada ya mshindi kukosewa.. (+Video)

on

Unaweza kukosea ukaomba radhi lakini watu wasiwe wepesi kukusamehe au kukuelewa kwamba umejikwaa kibinadamu… utata na kelele ziliibuka kwenye stage ya Planet Hollywood, Las Vegas Marekani saa chache zilizopita.

MC wa Miss Universe Final 2015 Marekani,  Steve Harvey

MC wa Miss Universe Final 2015 Marekani, Steve Harvey

Noma zaidi ni kwamba ishu haikuishia kwenye stage wala ukumbini, watu wakaingia mitandaoni kila mmoja akiongea la kwake huku wengi wakionekana kama hawajachukulia poa kosa la MC wa shughuli hiyo, Steve Harvey.

UNIVERSE II

Mrembo wa Philippines, Pia Alonzo Wurtzbach

Ishu ilikuwa ni kosa la MC huyo kumtaja mrembo Ariadna Gutierrez Arévalo kutoka Colombia kuwa ndiye mshindi, akavalishwa Taji na shangwe zikaanza… sekunde chache jamaa akaomba radhi kwamba hilo Taji sio lake, maana yake ni kwamba mrembo huyo sio mshindi, ila mshindi mwenyewe ni mrembo Pia Alonzo Wurtzbach kutoka Ufilipino, na Ariadna kutoka Colombia ni mrembo kwenye nafasi ya pili Miss Universe 2015.

Kipande cha video na tukio lote hivi hapa mtu wangu kama ulipitwa na hii

Soma na hizi

Tupia Comments