Michezo

Beki wa Manchester United kufanyiwa upasuaji kwa mara ya pili (+Pichaz&Video)

on

Beki wa klabu ya Manchester United Luke Shaw ambaye alivunjika mguu katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya klabu ya PSV Eindhoven ya Uholanzi, anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa pili siku ya Ijumaa.

Beki huyo wa kimataifa wa Uingereza anayekipiga katika klabu ya Manchester United alivunjika mguu mara mbili baada ya kufanyiwa tackling na beki wa PSV Hector Moreno dakika ya 15 ya mchezo. Baada ya kupata majeraha hayo Luke Shaw alipelekwa katika hospitali ya St Anna Ziekenhuis.

Luke-Shaw-Injury-In-Champions-League-match

Ila taarifa zilizotoka ni kuwa beki huyo aliyevunjika mara mbili mguu wake wa kulia, atafanyiwa upasuaji wa pili siku ya Ijumaa ya September 18, baada ya kufanyiwa uchunguzi. Stori kutoka talksport.com inasema kuvunjika kwa beki huyo kunaweza mfanya akae nje ya uwanja katika kipindi cha miezi sita. Lakini beki huyo bado yupo Uholanzi kwa matibabu.

Hii ni video ya tukio lililopekea Luke Shaw kuvunjika

https://youtu.be/jJDH4lapQfI

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata piausisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments