Stori Kubwa

Jamaa alisinzia kwenye sehemu inayowekwa mizigo ndani ya ndege, kilichofuatia hapo ni ishu..

on

Alaska 737-700 WL N622AS (90)(Grd) SEA (MBI)(46)-M

Ishu ilianzia pale ambapo ndege ilikuwa imeruka kama dakika 14 hivi Uwanja wa Seattle, Marekani.. Rubani mmoja akahisi kwamba kuna mlio wa kitu tofauti toka kwenye sehemu ambayo inawekwa mizigo ndani ya ndege hiyo.

Marubani wa ndege hiyo ilibidi waombe dharura kuirudisha ndege uwanjani hapo kwa kuwa walihisi sauti ya kitu wanayoisikia toka kwenye chumba hicho cha mizigo itakuwa ni mtu.

alaska-airlines

Ndege hiyo ilipotua uwanja wa Seattle-Tacoma

Baada ya ndege hiyo kutua watu jamaa alitoka kwenye chumba hicho ambacho huwa wanawekwa wanyama wanaposafirishwa.. anasema alikuwa amesinzia na hakuwa na habari na chochote kinachoendelea.

21.si

Mfanyakazi huyo alipotoka ndani ya ndege hiyo

Taarifa iliyotolewa na shirika la ndege hiyo imesema kuwa mfanyakazi huyo alipimwa lakini hakuwa ametumia kilevi chochote wala hakutumia dawa yoyote.. ndege hiyo aina ya Boeing 737, iliyokuwa na abiria 170 ilikuwa imeruka kwa dakika 14 angani ikielekea Los Angeles kabla ya kugundua kuwa kuna huyo jamaa ambaye alikuwa ammesinzia kwenye sehemu ya mizigo ya ndege hiyo.

millardayo.com ndio sehemu yako kuzipata story zote mtu wangu, unaweza kuwa karibu zaidi na mimi kwa kujiunga kwenye Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook

Soma na hizi

Tupia Comments