Mix

Upasuaji wa maumbile wapelekea mwanamke kufariki

on

SurgeryMwanamke mmoja amefariki wakati akifanyiwa upasuaji wa kurekebisha maumbile.

Mwanamke huyo raia wa Uingereza mwenye umri wa miaka 24 amefariki nchini Thailand alikokwenda kufanyiwa upasuaji huo, ambapo taarifa kutoka nchini humo zinasema baada ya kupatiwa vidonge vya usingizi mapigo yake ya moyo yalisimama.

Taarifa kutoka Thailand zinasema upasuaji huo ni wa awamu ya pili kufanyiwa, baada ya kutoridhiwa na matokeo ya upasuaji wa awali.

Waziri wa afya Boonruang Triruangworawat amesema jitihada zilizofanywa kuokoa maisha ya msichana huyo hazikusaidia.

Daktari aliyekuwa akimfanyia upasuaji huo aliyefahamika kwa jina la Dk. Sompob Sansiri anashikiliwa na polisi, huku serikali ikitangaza kuifungia kliniki alipokuwa akifanyia upasuaji kwa siku 60 kwa ajili ya kupisha uchunguzi.

Inasemekana kuwa unafuu wa huduma hiyo unapelekea watu wengi kutoka nchi za Ulaya kukimbilia Thailand licha ya kuripotiwa kutokea vifo vingi vya wateja wake.

Tupia Comments