Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Camilius Wambura amekanusha kuhusu taarifa zinazodai kwamba Hamza aliwashambulia Askari kwasababu walimdhulumu madini yake na kusema Hamza hakuwa na pesa wala hakuwa na madini huku akisisitiza kuwa uchunguzi umeonesha kuwa Hamza alikuwa ni Gaidi na mfia Dini.
“Hamza hakuwa na madini wala hakuwa na pesa na hakuwa na nafasi yoyote ya kumiliki madini wala pesa”– DCI Wambura
“Mbali ya kwamba Watu wengi wameongea kwamba Hamza alikuwa anamiliki migodi ya madini kule Chunya na maeneo ya Makongolosi lakini uchunguzi wetu umebaini hali hiyo ya maisha ilikwisha simama muda mrefu na Hamza alikuwa kwenye nafasi ya Magaidi wanaoamua kuifia Dini”- DCI Wambura
UPELELEZI WA TATU SAKATA LA HAMZA “ALIWASHAMBULIA ASKARI WA KWANZA AKACHUKUA SILAHA ZAO”