Top Stories

Upelelezi wa tatu sakata la Hamza “alishambulia Askari wa kwanza akachukua Silaha zao” (video+)

on

Siku chache tangu kuuawa kwa Hamza na polisi August 25, 2021 baada ya kuwaua kwa risasi Askari watatu na Mlinzi mmoja wa kampuni binafsi ya ulinzi jirani ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Camillius Wambura amezungumza leo Mkoani Mwanza na kusema uchunguzi uliyofanywa na Polisi umebaini kwamba Hamza Mohammed alikuwa Gaidi wa kujitoa mhanga.

“Kumekuwa na argument mbalimbali kwamba ni kwanini Hamza aliwashambuliwa Askari pekee, ni kweli aliwashambulia Askari wa kwanza akachukua silaha zao, akashambulia Askari mwingine wa usalama Barabarani akataka kwenda kumshambulia Askari mwingine anayelinda Ubalozi wa Ufaransa hakufanikiwa, Gari la Askari lilipopita pia alilishambulia”-DCI Wambura

Ayo TV & Millardayo.com imekusogezea hii video hapa ufahamu zaidi Upelelezi wa tatu kuhusu sakata la Hamza.

UPELELEZI WA PILI SAKATA LA HAMZA “HAMZA HAKUDHULUMIWA MADINI NA POLISI, NI MFIA DINI, HANA HELA”

Soma na hizi

Tupia Comments