Mix

Mambo matano yaliyosababisha hotuba ya upinzani kukataliwa Bungeni leo

on

May 15 2106 wizara ya mambo ya ndani ya nchi ilikuwa ikiwasilisha hotuba yake ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2016/2017

Taratibu huwa baada ya Wizara husika kuwasilisha hotuba yake hutolewa nafasi kwa kambi ya upinzani bungeni nayo kuwasilisha hotuba yake lakini mambo yakawa tofauti baada ya mwenyekiti wa bunge kuzuia kusomwa kwa hotuba hiyo mpaka kwanza kamati ya Kanuni ya Bunge iipitie..

Baada ya kuipitia mwenyekiti akaitaka kambi ya upinzani kuondoa baadhi ya maneno kwenye hotuba hiyo yaliyodaiwa kuwa yamekiuka kanuni na taratibu za bunge, maneno hayo ni pamoja na mkataba tata wa Lugumi, uuzwaji wa nyumba uliomtaja Rais John Magufuli moja kwa moja, rushwa na bunge kutumika kuwalinda watuhumiwa, tabia ya Rais na usalama wa nchi na mwisho ni kuwataja viongozi wa juu wa serikali kwa maneno ya dhihaka.

Godbless Lema msemaji wa kambi ya upinzani ambaye ni mbunge wa Arusha mjini akakataa kuyaondoa maneno hayo na kuacha kuisoma ambapo alipotoka nje ya bunge akaongea haya maneno kwenye hii video hapa chini.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments