Michezo

Urais wa TFF Mwanamke mmoja ajitokeza

on

Hawa Mniga ndio mwanamke pekee hadi sasa ambaye amejitokeza kugombea nafasi ya Urais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) katika Uchaguzi Mkuu wa August 7 2021 jijini Tanga.

Hawa Mniga kwa sasa ni Mkurugenzi wa Huduma wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) lakini kabla ya hapo amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za utumishi wa umma kama mjumbe wa kamati ya ajira ya TFF, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nzega Tabora na Meneja Rasilimali watu Kampuni ya magazeti ya Serikali (TSN).

Rais wa sasa Wallace Karia anatetea kiti chake sambamba na wagombea wengine waliojitokeza kuwania nafasi hiyo ni Mbunge wa Kinondoni Abbas Tarimba, Ally Mayay, Evans Mgeusa, Oscar Oscar, Zahir Mohamed Haji, Deogratus Mutungi.

Soma na hizi

Tupia Comments