Habari za Mastaa

Hivi ndivyo Urban Fresh Jitambue ilivyokuwa

on

DSC_0490Tamasha la Urban Fresh Jitambue lililokuwa na moto usemao Jiamini U Can Do It  limemalizika kwa wanafunzi mbalimbali kupata chakula cha ubongo kutoka kwa wasemaji mbali mbali waliokuwepo siku ya leo

DSC_0613Miongoni mwa wasemaji waliotoa chakula cha ubongo leo ni pamoja na Ay,Jokate,B dozen,Adam Mchomvu pamoja na mimi mtu wako wa nguvu millard ayo,miongoni mwa vitu vingi vilivyozungumza na wasemaji mbali mbali ni juhudi katika masomo,kujituma katika kazi mbalimbali na kumuomba Mungu.

DSC_0501

Binafsi nilitoa mfano wa jinsi sehemu nilizowahi kufanya kazi,pamoja na malipo madogo niliyowahi kuwa nalipwa kipindi hicho lakini sikukata tamaa niliamua kuongeza juhudi kwenye kazi yangu nikiamini kuna siku Mungu atanisaidia,hivyo tujifunze sana kujitolea zaidi kuliko kutegemea malipo makubwa ya kazi.

DSC_0551Alichokizungumza Bdozen toka Xxl ya Clouds Fm ni kusali sana yaani Kumuomba Mungu,kuwasikiliza wazazi maana ni Mungu wa pili duniani na kusoma kwa bidii kwenye masomo huku akitoa mfano wa jinsi yeye anavyoweza kukutana na mameneja masoko na wanavyoweza kuelewana pengine bila elimu ingekua ngumu.

DSC_0775Msanii Fid Q alitoa dili ya kuondoka na Dj mmoja ambaye pia walichuana na kisha Dj mmoja alipata dili ya kwenda kwenye mafunzo ya U-dj kwa ajili ya Cheusi Dawa tv,mbali na Fid Q pia mwanadada Jokate pia alimpata mtu mmoja kwa ajili ya mitindo ambapo dada huyo aliweza kufuma gauni kwa kutumia uzi.

DSC_0457Kwa Ay aliondoka na wasanii wawili wa kike na wakiume kwa ajili ya kuwafundisha muziki na kama wakifuzu kuwaingiza moja kwa moja kwenye kampuni yake ya Unit Intertainment.

DSC_0427Baada ya haya yote kuisha List ndefu ya wasanii ndefu ilipata nafasi ya kulishambulia jukwaa akiwemo Madee,Young Killer,Navy Kenzo,M-rap,Rich mavoko,Vanessa Mdee,Bob Junior,Kala Jeremiah,Shettah na wasanii wengine wengi.

Hizi ni baadhi ya picha za tukio hili lilivyofana.

DSC_0576

DSC_0571

DSC_0555

DSC_0525

DSC_0420

DSC_0344

DSC_0710

DSC_0688

DSC_0669

DSC_0726

DSC_0590

DSC_0588

DSC_0366

Tupia Comments