Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa Italia Fabrizio Romano ambaye amekuwa akiripoti habari nyingi za uhakika kupitia ukurasa wake wa twitter.
Ameripoti kuwa Ureno wamefikia hatua ya kumfuta kazi Koch wao Mkuu Fernando Santos (68) siku chache baada ya kutolewa katika hatua ya robo fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco.
Fernando Santos amekuwa Kocha wa Ureno toka 2014-2022 na mwaka 2016 alifanikiwa kuipa Ureno taji lao la kwanza la michuano ya Euro.