Rais wa Urusi Vladimir Putin amewashukuru wanajeshi wake kwa michango waliyotoa katika uvamizi wa nchi yake nchini Ukraine. Pia amebainisha kuwa Urusi inafikia malengo yake.
Jana Jumapili Putin alitoa hotuba wakati wa hafla iliyofanyika kuadhimisha “Siku ya Mlinzi wa Taifa” katika Ikulu ya nchi hiyo.
Rais huyo aliwashukuru wanajeshi ambao wamepigana nchini Ukraine.
Alisema nchi inajivunia wao na michango waliyoitoa katika utetezi wa nchi yao.
Putin alitoa ujumbe wa video siku hiyo hiyo.
Ndani yake, alisema, “Leo, wakati ulimwengu unabadilika kwa kasi, njia yetu ya kimkakati ya kuimarisha na kuendeleza Jeshi bado haijabadilika.”
Pia alisema, “Tutaendelea kujenga uwezo wa mapambano wa jeshi la nchi kavu na la wanamaji.”