Kremlin inakanusha kuwa Urusi inasababisha njaa barani Afrika baada ya kujiondoa kwenye mpango wa nafaka na kuwa hauna maana.
Kremlin inasema uhaba wa chakula barani Afrika hauna uhusiano wowote na Urusi baada ya kujiondoa katika makubaliano yaliyoiruhusu Ukraine kusafirisha nafaka zake kwa usalama katika Bahari Nyeusi wakati wa vita.
Msemaji wa Kremlin Dimitry Peskov alikuwa akijibu ripoti ya mkuu wa Baraza la Usalama la Ukraine kwamba Moscow inasababisha njaa barani Afrika.
Kujiondoa kwa Urusi kumesimamisha kwa karibu usafirishaji wote wa nafaka wa Ukraine kwa njia ya bahari, lakini Peskov alisisitiza kwamba Urusi imesalia kuwa msambazaji wa kuaminika wa mkataba huo wa nafaka licha ya vikwazo vilivyowekwa na Marekani na Umoja wa Ulaya.