Nchi za Rwanda na Urusi zimetuma Wanajeshi na vifaa Jamhuri ya Afrika ya Kati ikiwa ni jitihada za kusaidia kupambana na vurugu wakati Taifa hilo likijiandaa kufanya Uchaguzi Mkuu Jumapili hii.
Vikosi vya Usalama pamoja na Askari wa kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa (UN) vimekuwa vikikabiliana na waasi waliodhibiti Miji na barabara nje ya Mji Mkuu wa Bangui.
Serikali inamshutumu Rais wa zamani, Francois Bozize, kupanga mapinduzi akishirikiana na baadhi ya makundi ya wapiganaji. Mahakama ilikataa ombi la Bozize kugombea tena Urais.