Michezo

Urusi yafungiwa kushiriki michezo yote

on

Taifa la Urusi limekumbana na changamoto kubwa kufuatia taifa hilo leo hii kutangazwa kufungiwa miaka minne kujihusisha na mchezo wowote ule wa ngazi ya kidunia.

Urusi imekumbana na adhabu hiyo baada ya ofisi ya wakala wa kuzuia dawa zisizoruhusiwa michezoni (World Anti-Doping Agency) kwa kubaini kuwa Urusi walifanya udanganyifu kuhusiana na matumizi ya dawa zisizoruhusiwa michezoni.

Adhabu hiyo kama haitokatiwa rufaa katika Mahakama ya kimichezo duniani (CAS) ndani ya siku 21 basi ni wazi itakuwa Urusi inakosa kushiriki michuano ya Olympic na Kombe la Dunia 2022.

 

Soma na hizi

Tupia Comments