Idadi ya raia waliouawa katika mapigano ya silaha na mitetemeko ya kibinadamu imeongezeka, na Umoja wa Mataifa ukihesabu karibu vifo 17,000 vilivyorekodiwa mwaka jana katika maeneo ya vita ikiwa ni pamoja na karibu watu 8,000 waliouawa nchini Ukraine pekee kuashiria ongezeko kubwa la asilimia 53 ya mauaji ya raia ikilinganishwa na 2021.
Akitaja idadi ya watu waliouawa katika vita vya Ukraine na Sudan, shule zilizoharibiwa nchini Ethiopia, na uharibifu wa miundombinu ya maji nchini Syria, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alisema Jumanne kwamba “ulimwengu unashindwa” kuwalinda raia.
Ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu ulinzi wa raia katika mizozo ya mwaka 2022 inaongeza kiwango kipya cha ongezeko la asilimia 53 ya vifo vya raia vilivyorekodiwa na Umoja wa Mataifa na kuongezeka kwa idadi ya watu waliolazimika kuyahama makazi yao kutokana na mizozo.
Ulimwenguni kote, idadi ya wakimbizi wanaolazimishwa kutoka makwao “kutokana na migogoro, ghasia, ukiukaji wa haki za binadamu na mateso” imefikia milioni 100, mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa aliongeza.