Raia tisini na wawili wa Marekani wamepigwa marufuku kuingia Urusi. Watu hao ni waathiriwa wa mzozo wa Ukraine. Moscow inawashutumu kwa kueneza habari za uwongo kuhusu vikosi vya jeshi la Urusi, na kushiriki katika “vita vya mseto” vilivyochochewa na Washington.
Wengi wao ni waandishi wa habari, walioajiriwa na vyombo vikuu vya habari vya Marekani. Wafanyakazi kumi na wanne wa Gazeti la Wall Street Journal, ikiwa ni pamoja na mhariri wake mkuu, Emma Tucker, waandishi wa habari watano kutoka Gazeti la New York Times, wanne kutoka Gazeti la Washington Post.
Lakini orodha hii pia inajumuisha wanajeshi, kama vile mkuu wa Kamandi ya Anga ya Juu ya Marekani, maprofesa wa vyuo vikuu, watendaji wa kampuni wanaohusishwa na sekta ya silaha, wanasiasa, wanasheria, waendesha mashtaka au wanachama wa mashirika ya kibinadamu.
Tunaikumbusha mamlaka ya Marekani kwamba bila shaka tutaadhibu kitendo chochote cha uadui, ikiwa kinahusisha kuhimiza mashambulizi ya kigaidi na Ukraine au kuingilia kati katika masuala ya ndani ya Shirikisho la Urusi, diplomasia ya Urusi imeandika.