Mix

Unasema DAR kuna kelele?? Cheki hii miji inayoongoza kwa kelele Marekani..

on

nyc-skyline

Moja ya ishu zilizojadiliwa Bungeni katika vikao vilivyofanyika ndani ya wiki hii ni suala la kelele ndani ya Miji Mikubwa TZ kam vile Dar.. Wabunge wakasema ikiwezekana kuwepo utaratibu wa kufungia kumbi za sherehe ambazo zinaongoza kwa kupiga muziki na kusababisha kero ya kelele.

Nimepita mitandaoni nikakuta hii list mtu wangu.. Hapa ni Miji mikubwa mitano inayoongoza kwa kelele Marekani.

.

No.1: Karibu New York mtu wa nguvu !! Huu ni moja ya Miji yenye watu wengi zaidi Marekani, mishemishe ni nyingi pia ikiwemo Utalii. Huu ni namba moja kwa kelele Marekani.

Detroit_Michigan_freecomputerdesktopwallpaper_1280

No.2: Detroit, Michigan. Unaambiwa isikushtue mji huu kuwa namba mbili kwa kuwa na makelele mengi kwa Marekani, unatajwa kuwa unaongoza pia kwa matukio ya uhalifu. Ukiingia hapa mtu wangu kaa macho.

DSC_0253

No.3: San Francisco, California. Utafiti uliofanywa na University of California, Berkeley unaonesha mtu mmoja kati ya watu sita wako kwenye hatari ya kuugua magonjwa ya moyo kutokana na kelele za magari.

Miami Beach street view, ocean Drive at 9th Street, South Beach, Miami Beach, Florida

No.4: Miami, Florida. Huu ni mji ambao uko kwenye list ya miji ya starehe zaidi Marekani. Sehemu kubwa ya malalamiko kuhusu kelele inasababishwa na kutua na kuruka kwa ndege, O’Hare International Airport ilikuwa inapokea ndege zaidi ya 2,500 kila siku mwaka 2015.

Hii ikitokea tukifanya utafiti Bongo unadhani mji upi utaongoza kwa kero ya kelele nyingi?

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Soma na hizi

Tupia Comments