Mix

Picha za Polisi waliomuua Mmarekani mweusi juzi zaonyeshwa ( tahadhari video zinatisha)

on

Yametokea mauaji ya Wanaume Wamarekani weusi wawili ndani ya siku mbili nchini Marekani ambapo wa kwanza alikua muuzaji wa CD aliyeuwawa kwa kupigwa risasi akiwa chini ya ulinzi wa Polisi wawili waliokua wamemlaza chini.

Polisi 2

Video ya mauaji ya kwanza ya Alton Sterling inaonyesha hakuwa na bunduki mikononi mwake kama ilivyodaiwa na Polisi wakati wakiwa wamemuweka chini ya ulinzi, video yenyewe ni hii hapa chini (tahadhari inatisha)

Mauaji ya pili yametokea kwa Philando Castile aliyekua akiendesha gari dogo akiwa na mpenzi wake na mtoto wao ambapo alisimamishwa na Polisi na kuuwawa kwa kupigwa risasi sekunde chache baadae huku Polisi akionekana kujihami kutokana na Mwanaume huyo kutaka kutoa leseni yake mfukoni lakini Polisi akiamini alikua akitaka kutumia bastola.

Mama watoto wake ambaye alikua nae kwenye gari alianza kurusha live kinachoendelea kupitia ukurasa wake wa Facebook kama inavyoonekana hapa chini, (tahadhari inatisha)

ULIPITWA NA EXCLUSIVE YA NYUMBA YA MILIONI 700 WANAYOIJENGA NAVY KENZO? TAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments