AyoTV

‘Wanasema alikuwa Modo leo ni mwanasiasa inahusu…? – DC JOKATE

on

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo amewataka wanawake wasiogope kuitwa wanakimbele mbele kutokana na kuchangamkia fursa, huku akisema wapo wanaomsema kwamba alikuwa ‘Model’ lakini leo kawa mwanasiasa.

DC Jokate ameyasema hayo katika Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Wanawake ambapo amesema hawajahi kuamini anashindwa kufanya chochote anachoamua dunia, kwani hilo limechangiwa na malezi kutoka kwa wazazi wake.

“Nawapa changamoto wanawake wenzangu kwani mara nyingi wanaume ni wachoyo aidha ni wachoyo ama wanaogopa nguvu ya mwanamke, kwani mara nyingi haki zinapiganiwa na hatupewi mikononi tukamate fursa na tujifunze na tusipende kutosheka,”amesema.

Pia amesema ili wanawake wakamate nafasi mbalimbali za uongozi lazima wajifunze, wawe na ujuzi, elimu na maarifa.

“Wanawake waiogope kujitokeza kuitwa wanakimbele mbele kwani wanasema huyu aliokuwa Modo na leo mwanasiasa…inahusu…mie nawaambia inahusu kwani uwezo ninao maamuzi ninayo nitafanya kazi kwa bidii zote,”amesema.

DC JOKATE ALIVYOTAJA SIFA TATU KUHUSU WAZIRI MHAGAMA ‘WEWE NI MREMBO’

Soma na hizi

Tupia Comments