Duniani

Mtoto aliyekamatwa na saa wakidhani ni bomu harudi tena Shule? Boss wa Facebook nae kaandika haya..

on

Stori bado inagusa kwenye vichwa vya habari Duniani, September 16 nilikusogezea stori ya Ahmed Mohamed mtoto mwenye umri wa miaka 14 ambaye alikamatwa Shuleni na kupelekwa Polisi baada ya kukutwa na saa aliyoibuni yeye mwenyewe lakini Walimu na Polisi walidhani ni Bomu !!

Siku iliyofuatia Rais wa Marekani, Barack Obama aliguswa, akaandika kwenye ukurasa wake Facebook kwamba anamkaribisha ndani ya Ikulu ya Marekani kama njia ya kufanya watoto wapende somo la Sayansi.

OBAMA

Ahmed alikuwa mwanafunzi wa Shule ya MacArthur High School iliyoko Irving, Texas Marekani… kingine kuhusu yeye leo ni kwamba Baba wa Ahmed, Mohamed Elhassan Mohamed amethibitisha kwamba Familia haiko tayari kumrudisha Ahmed Shuleni hapo.

Japo Polisi waliridhika na Uchunguzi kwamba kifaa alichokamatwa nacho sio Bomu, msimamo wa Shule uko palepale… wanasema hairuhusiwi mwanafunzi kuja na vitu ambavyo vimekatazwa Shuleni hapo, kwa hiyo hata hiyo ya Ahmed kukamatwa hawako tayari kuomba radhi.

Ahmed

Boss mwenyewe wa Facebook, Mark Zuckerberg amempongeza Ahmed kwa kipaji chake huku akisema kwamba mtoto huyo alitakiwa kupongezwa na sio kukamatwa na Polisi, kwa sababu Dunia inawahitaji zaidi watu kama yeye.

Zuck Boy

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments