Mix

Usajili: Huyu ndio staa mpya aliyesajiliwa na Man United leo hii

on

IMG_6909.PNG

Leo ndio siku ya mwisho ya usajili barani ulaya na kila klabu ipo katika harakati za kuimarisha timu zao.

Klabu ya Manchester United leo hii imezishinda Manchester City, Real Madrid, Arsenal katika mbio za kusaka saini ya mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia Radamel Falcao.

United ambayo juzi ilikamilisha usajili wa Angel Di maria, leo imekamilisha usajili wa Falcao kwa mkataba wa mkopo wa mwaka 1 ambao una gharama ya £12m.

Falcao anategemea kutua jijini Manchester leo jioni kwa ajili ya vipimo vya afya na kusaini mkataba.

Tupia Comments