Michezo

Usajili wa De Gea na Navas waelekea kukamilika usiku huu

on

Siku ya mwisho ya usajili barani ulaya inazidi kunoga, inaripotiwa kwamba vilabu vya Manchester United vimefikia makubaliano juu ya biashara ya wachezaji David De Gea na Kylor Navas.  

Baada ya kujaribu kumsajili De Gea kwa muda wote wa dirisha la usajili hatimaye Madrid wamefikia makubaliano na United juu ya usajili wa David De Gea kwenda Santigo Bernabeu katika dili ambalo linatajwa kumhusisha Keylor Navas kuhamia Old Trafford.  

Usajili huo bado haujakamilika lakini inaripotiwa Madrid watailipa Manchester United kiasi cha 40m euros (£29m).

Kwa muda wote wa dirisha la usajili Man United imekuwa ikisisitiza kulipwa ada ya uhamisho itakayovunja rekodi kwa uhamisho wa magolikipa au dili hiyo imhusishe Sergio Ramos, lakini mwisho wa siku Kylor Navas ndio ataenda Theater of Dreams.

Tupia Comments